← Nafasi zote zilizo wazi

Usafirishaji na ugavi · Haijatajwa

Chanzo rasmi

DEREVA DARAJA II (DRIVER II)

HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE

TanzaniaWanaoanza · Haijatajwa5 nafasi zilizo waziMwisho 2026-10-30Imekaguliwa 18 Okt 2026
Illustration of a warehouse packing desk with boxes and a barcode scanner.

Imechapishwa na mwajiri

Kuhusu nafasi hii

Muhtasari wa nafasi

1.0 DEREVA DARAJA II (DRIVER II) - Nafasi 5

Soma nafasi yote

KAZI

i Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari; ii Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi; iii Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari; iv Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; v Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali; na vi Kufanya usafi wa Gari;

MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE

Page 1 of 4

MASHARTI YA JUMLA

Page 2 of 4

Waombaji wote lazima wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi umri wa miaka 45. Hata hivyo, kwa nafasi za ndani ya Taasisi za Kijeshi: Waombaji wa nafasi zisizo za shahada wasizidi umri wa miaka 25. Waombaji wa nafasi za shahada wasizidi umri wa miaka 30. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na

Mwanasheria/Wakili

Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma,

WASIOMBE

na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba

CAC45/257/01/D/140

wa tarehe 30 Novemba 2010. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-

Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates

Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) "Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). Kwa waombaji wa kada zinazohitaji 'GPA' waliosoma nje ya Tanzania waambatishe cheti cha ukokotozi wa 'GPA' kutoka TCU. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe

30 Oktoba, 2026

Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

Mkurugenzi Mtendaji

Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe

Page 3 of 4

S.L.P 443, Kigoma

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ . (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa '

Recruitment

Portal

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili

HAYATAFIKIRIWA

Waombaji wote wa kazi wanakumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira unazingatia misingi ya haki, usawa, na uwazi, kwa kuzingatia sifa stahiki zilizoainishwa katika tangazo la kazi husika na muundo wa utumishi wa idara inayohusika. Limetolewa na:

HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE

Page 4 of 4

Angalia tangazo na uombe