- Mwajiri
- Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
- Eneo
- Tanzania (specific workplace not stated)
- Tarehe ya mwisho
- 2026-09-23
- Nafasi
- 1
- Chanzo kilikaguliwa
- 2026-09-23
Sifa na majukumu
1.0 DEREVA DARAJA II (DRIVER II) - Nafasi 1
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
ii. Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
iv. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
v. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali; na
vi. Kufanya usafi wa Gari;
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya
uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1)
bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata
madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari
(Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA
MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
1.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGS B
Masharti ya jumla
MASHARTI YA JUMLA
1. Waombaji wote lazima wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi
umri wa miaka 45. Hata hivyo, kwa nafasi za ndani ya Taasisi za Kijeshi:
Waombaji wa nafasi zisizo za shahada wasizidi umri wa miaka 25.
Waombaji wa nafasi za shahada wasizidi umri wa miaka 30.
2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
3. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili.
4. Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba
CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
5. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti
vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
6. "Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato
cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
7. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). Kwa waombaji wa
kada zinazohitaji 'GPA' waliosoma nje ya Tanzania waambatishe cheti cha ukokotozi
wa 'GPA' kutoka TCU.
8. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
9. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
10. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 23 Septemba, 2026.
11. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti
vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
S.L.P 332, Kigoma
12. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)
kupitia anuani ifuatayo;https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye
tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment
Portal').
13. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
14. Waombaji wote wa kazi wanakumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea
rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira
unazingatia misingi ya haki, usawa, na uwazi, kwa kuzingatia sifa stahiki
zilizoainishwa katika tangazo la kazi husika na muundo wa utumishi wa idara
inayohusika.
Limetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA