Looking for remote work in Africa? Find it on workafro.com →
← Nafasi zote zilizo wazi

Usafirishaji na ugavi · Haijatajwa

Chanzo rasmi

Dereva Daraja la II

HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI

TanzaniaWanaoanza · Haijatajwa7 nafasi zilizo waziMwisho 2026-11-10Imekaguliwa 7 Nov 2026
Illustration of a warehouse packing desk with boxes and a barcode scanner.

Imechapishwa na mwajiri

Kuhusu nafasi hii

1.1 MAJUKUMU NA KAZI

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari; ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbali mbali kwenye safari za kikazi; iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari; iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali; v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; vi. Kufanya usafi wa gari; vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

Soma nafasi yote

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye elimu ya kidato cha Nne (Form IV) na leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali,pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Vilevile wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na vyuo vyovyote vinavyotambuliwa na serikali.

MASHARTI YA JUMLA

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45; ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma; iii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilich othibitishwa na

Mwanasheria/Wakili;

iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza ( Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika; v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya ta aluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/ Degre e/ Advanced Diploma/ Diploma/ Certificates, -Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI , - Computer Certificate, -Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards); vi. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)

HAVITAKUBALIWA;

vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na

NACTE);

viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingat ia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe

30 Novemba, 2010;

x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria; xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 10 Novemba, 2026; MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

HAI

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira Recruitment Portal kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Seckretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘ Recruitment Portal’).Aidha, maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA. Limetolewa na;

Angalia tangazo na uombe