- Mwajiri
- HALMASHAURI YA MJI MAFINGA
- Eneo
- Tanzania (specific workplace not stated)
- Tarehe ya mwisho
- 2026-09-24
- Nafasi
- 1
- Chanzo kilikaguliwa
- 2026-09-23
Sifa na majukumu
1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II - NAFASI 1
1.1 KAZI NA MAJUKUMU
i. Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye Regista
(Incomming);
ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence
Register);
iii. Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers);
iv. Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji;
v. Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji;
vi. Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling
Cabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa; na
vii. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani nan je ya Taasisi (File tracking).
1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada
(NTA level 6) katika fani ya Masjala kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi
wa Kompyuta.
Ofisi ya Mkurugenzi, Mtaa wa Mtangani - Luganga, S.L.P. 76 Mafinga – Iringa: Simu: +255 026 2772393
Nukushi: +255 026 2772393 Barua pepe:td@mafingatc.go.tz; Tovuti: www.mafingatc.go.tz
1.1.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGS C
Masharti ya jumla
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na
usiozidi miaka 45 ;
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha
kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti
ya Ajira Katika Utumishi wa Umma.
iii. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae)
Ofisi ya Mkurugenzi, Mtaa wa Mtangani - Luganga, S.L.P. 76 Mafinga – Iringa: Simu: +255 026 2772393
Nukushi: +255 026 2772393 Barua pepe:td@mafingatc.go.tz; Tovuti: www.mafingatc.go.tz
yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe
(E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
iv. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia katika
kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri
wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani
na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa
kuaminika;
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia
kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
husika.Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, - Cheti cha
mtihani wa Kidato cha IV na VI, - Computer Certificate, - Vyeti vya Kitaaluma
(Professional Certificate from Respective Boards);
vii. “Testmonial”, ‘‘Provisional Results”, “Statement of results”, hati ya matokeo ya Kidato
cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana
kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za
kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo
katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
x. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 24 Septemba, 2026.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na
vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: -
Ofisi ya Mkurugenzi, Mtaa wa Mtangani - Luganga, S.L.P. 76 Mafinga – Iringa: Simu: +255 026 2772393
Nukushi: +255 026 2772393 Barua pepe:td@mafingatc.go.tz; Tovuti: www.mafingatc.go.tz
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji Mafinga,
S.L.P. 76,
MAFINGA.
xi. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)
kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye
tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment
Portal'). Aidha, Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
Limetolewa na:
MKURUGENZI WA MJI
HALMASHAURI YA MJI
MAFINGA