- Mwajiri
- HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO
- Eneo
- Tanzania (specific workplace not stated)
- Tarehe ya mwisho
- 2026-09-23
- Nafasi
- 4
- Chanzo kilikaguliwa
- 2026-09-23
Sifa na majukumu
2.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (OFFICE MANAGEMENT SECRETARY GRADE II) - Nafasi 4
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri;
ii. Kupokea wageni na kuwasikiza shida zao na kuwaelekeza wanapoweza
kusaidiwa;
iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za
Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya
kazi;
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu
husika;
vi. .Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mablimbali;
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; naix.Kufanya kazi zingine
atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six)
wenye Stashahada (NTA Level 6) ya Uhazili (Secretarial Studies). Aidha, wawe
wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 (80.w.p.m) kwa
dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word,
Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
2.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGS C
Masharti ya jumla
MASHARTI YA JUMLA
1. Waombaji wote lazima wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi
umri wa miaka 45. Hata hivyo, kwa nafasi za ndani ya Taasisi za Kijeshi:
Waombaji wa nafasi zisizo za shahada wasizidi umri wa miaka 25.
Waombaji wa nafasi za shahada wasizidi umri wa miaka 30.
2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
3. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili.
4. Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba
CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
5. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti
vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
6. "Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato
cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
7. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). Kwa waombaji wa
kada zinazohitaji 'GPA' waliosoma nje ya Tanzania waambatishe cheti cha ukokotozi
wa 'GPA' kutoka TCU.
8. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
9. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
10. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 23 Septemba, 2026.
11. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti
vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
S.L.P. 03,
KAKONKO
12. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)
kupitia anuani ifuatayo;https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye
tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment
Portal').
13. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
14. Waombaji wote wa kazi wanakumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea
rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira
unazingatia misingi ya haki, usawa, na uwazi, kwa kuzingatia sifa stahiki
zilizoainishwa katika tangazo la kazi husika na muundo wa utumishi wa idara
inayohusika.
Limetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO