Looking for remote work in Africa? Find it on workafro.com →
← Nafasi zote zilizo wazi

Utawala · Haijatajwa

Chanzo rasmi

Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (Office Management Secretary Grade II)

HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI

MoshiWanaoanza · Haijatajwa4 nafasi zilizo waziMwisho 2026-11-20Imekaguliwa 7 Nov 2026
Illustration of an office desk with a laptop and notebook.

Imechapishwa na mwajiri

Kuhusu nafasi hii

Muhtasari wa nafasi

2.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (OFFICE MANAGEMENT SECRETARY GRADE II) - Nafasi 4

Soma nafasi yote

2.1 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri; ii. Kupokea wageni na kuwasikiza shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa; iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine; iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi; v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu husika; vi. .Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika; vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mablimbali; viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; naix.Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

2.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six) wenye Stashahada (NTA Level 6) ya Uhazili (Secretarial Studies). Aidha, wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 (80.w.p.m) kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E -mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MASHARTI YA JUMLA

Page 3 of 4

  • Waombaji wote lazima wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi

umri wa miaka 45. Hata hivyo, kwa nafasi za ndani ya Taasisi za Kijeshi: Waombaji wa nafasi zisizo za shahada wasizidi umri wa miaka 25. Waombaji wa nafasi za shahada wasizidi umri wa miaka 30.

  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa

kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na

Mwanasheria/Wakili

  • Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na

wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti

vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-

Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates

Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

  • "Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato

cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na

kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). Kwa waombaji wa kada zinazohitaji 'GPA' waliosoma nje ya Tanzania waambatishe cheti cha ukokotozi wa 'GPA' kutoka TCU.

  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba

isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za

kisheria.

  • Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 20 Novemba, 2026.
  • Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti

vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

Mkurugenzi Mtendaji

Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

S.L.P 3003, Kilimanjaro

Page 4 of 4

  • Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)

kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ' Recruitment

Portal')

  • Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili

HAYATAFIKIRIWA

  • Waombaji wote wa kazi wanakumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea

rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira unazingatia misingi ya haki, usawa, na uwazi, kwa kuzingatia sifa stahiki zilizoainishwa katika tangazo la kazi husika na muundo wa utumishi wa idara inayohusika. Limetolewa na:

Angalia tangazo na uombe