Nyingine · Haijatajwa
Chanzo rasmiMwandishi Mwendesha Ofisi II

Imechapishwa na mwajiri
Kuhusu nafasi hii
2.1 KAZI NA MAJUKUMU
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri; ii. Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa; iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine; iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi; v. Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara / Kitengo/ Sehemu husika, Kukusanya, kutunza na ku yarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika; vi. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali; vii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi; viii. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
Soma nafasi yote
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne au Sita mwenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno100 kwa dakika moja na kupata program za Kompyuta za ofisi k ama vile: Word, Excel, Powerpoint, internet, email na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45; ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma; iii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilich othibitishwa na
Mwanasheria/Wakili;
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza ( Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika; v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya ta aluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/ Degre e/ Advanced Diploma/ Diploma/ Certificates, -Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI , - Computer Certificate, -Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards); vi. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA;
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na
NACTE);
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingat ia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe
30 Novemba, 2010;
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria; xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 10 Novemba, 2026; MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
HAI
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira Recruitment Portal kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Seckretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘ Recruitment Portal’).Aidha, maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA. Limetolewa na;