Mwajiri
KUHAMIA SEKRETARIETI YA AJIRA
Eneo
Tanzania (mahali pa kazi hapajatajwa)
Tarehe ya mwisho
12 Oktoba 2026
Nafasi
1
Chanzo kilikaguliwa
29 Septemba 2026
Tarehe ya mwajiri
29 Septemba 2026

Sifa na majukumu

1.0 AFISA SHERIA MWANDAMIZI - NAFASI 01
1.2 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutoa ushauri na msaada wa kisheria kwa Sekretarieti ya Ajira;
ii. Kutoa mapendekezo ya maboresho katika uandaaji wa miswaada ya kisheria/
sheria, sheria ndogo pamoja na kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali;
iii. Kufuatilia mashauri yaliyopo Mahakamani kwa kushirikiana na Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
iv. Kusimamia uandaaji na mapitio ya nyaraka mbalimbali za kisheria;
v. Kushiriki katika majadiliano na vikao mbalimbali vinavyohitaji utaalamu wa
kisheria na;
vi. Kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kushughulik ia
mashauri ya madai ya kiraia yanayohusisha Sekretarieti.
1.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Mtumishi wa Umma mwenye Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) kutoka katika taasisi
zinazotambuliwa na Serikali, pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka saba (7) ka tika
eneo linalohusiana na kazi hiyo . Vilevile, mwombaji lazima awe amehudhuria na kufaulu
mafunzo ya uanasheria kwa Vitendo (Internship) au Shule ya Sheria Tanzania. Aidha
mwombaji anatakiwa awe amesa jiliwa kama wakili wa mahakama K uu.Vilevile, mwombaji
awe mtumishi wa Umma aliyefanya kazi kwa Mwajiri wa sasa kwa kipindi cha muda
usiopungua miaka mitatu na awe tayari kujigharamia gharama za uhamisho.
1.4 NGAZI YA MSHAHARA
Utazingatia viwango vya mshahara vilivyoainishwa kwenye Muundo wa Maendeleo ya
Utumishi wa Taasisi.

Masharti ya jumla

MASHARTI YA JUMLA.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania ambao ni watumishi wa Umma;
ii. Mwombaji ni lazima awe mtumishi wa Umma aliyefikia ngazi ya Mwandamizi;
iii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na
wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu
walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma;
iv. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili;
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza ( Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika;
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti
vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzailiwa, vyeti vya
Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
husika;Postgraduate/Degree/Advanced, Diploma/Diploma/Certificates, Cheti
cha mtihani wa Kidato cha IV na VI na Computer Certificate.
vii. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato
cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA;
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa
na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET);
ix. Watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria;
x. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 12 Oktoba, 2026.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa ,
iliyopitishwa na mwajiri pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua
hiyo ielekezwe kwa
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
MTAA WA MAHAKAMA,
ENEO LA TAMBUKARELI,
S. L. P. 2320,
DODOMA.
xi. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo;http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana
kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa
(‘Recruitment Portal’). Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu
ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Limetolewa na;
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA