- Mwajiri
- HALMASHAURI YA WILAYA MBOZI
- Eneo
- Tanzania (specific workplace not stated)
- Tarehe ya mwisho
- 2026-10-01
- Nafasi
- 5
- Chanzo kilikaguliwa
- 2026-09-23
Sifa na majukumu
2.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 05
2.1 KAZI NA MAJUKUMU.
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
iii. Kufanya matengenezo madogo ya gari;
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
vi. Kufanya usafi wa gari; na
vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
2.2.1 SIFA ZA MWOMBAJI.
Kuajiriwa mwenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya
uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1)
bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyompatia sifa ya kupata madaraja
husika. Vilevile, awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic
Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali.
2.2.2 NGAZI YA MSHAHARA
TGS B1
Masharti ya jumla
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi
miaka 45.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail
Address) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili, ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita, kwa
wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika: Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/
Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na cha Sita,
Computer Certificate, - Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from
Respective Boards).
v. “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo ya
kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA.
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
vii. Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa
KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja
husika.
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xi. Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za
kisheria.
xii. Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa
kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya
Ardhi.
xiii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 01 Oktoba, 2026.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na
vyeti vya Elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi,
S.L.P. 3,
MBOZI.
xiv. Maombi yote ya kazi yatumwe katika mfumo wa Kielektroniki wa ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana
katika Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa
“Recruitment Portal”).
xv. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
Limetolewa na;
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI