Mwajiri
HALMASHAURI YA MJI MAFINGA
Eneo
Tanzania (specific workplace not stated)
Tarehe ya mwisho
2026-09-24
Nafasi
2
Chanzo kilikaguliwa
2026-09-23

Sifa na majukumu

2.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II - NAFASI 2
2.1 KAZI NA MAJUKUMU.
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida;
ii. Kusaidia kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaelekeza
sehemu wanazoweza kushughulikiwa;
iii. Kusaidia kutunza taarifa / kumbukumbu za Matukio, Miadi, Wageni, tarehe za vikao, Safari za
Mkuu wake na ratiba za kazi zingine zilipangwa kutekelezwa;
iv. Katika Ofisi anayofanyia kazi na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika;
v. Kusaidia kutatua na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote
kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo Ofisini;
vi. Kusaidia kufikisha maelezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na kumtaarifu
kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao;
vii. Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo na
kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika; na
viii. Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
2.2.1 SIFA ZA KUAJIRIWA
Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) pamoja na
Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili kutoka chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na
Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na awe amepata mafunzo ya programu za
kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, Email na Publisher.
2.2.2 NGAZI YA MSHAHARA
TGS C

Masharti ya jumla

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na
usiozidi miaka 45 ;
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha
kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti
ya Ajira Katika Utumishi wa Umma.
iii. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae)
Ofisi ya Mkurugenzi, Mtaa wa Mtangani - Luganga, S.L.P. 76 Mafinga – Iringa: Simu: +255 026 2772393
Nukushi: +255 026 2772393 Barua pepe:td@mafingatc.go.tz; Tovuti: www.mafingatc.go.tz
yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe
(E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
iv. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia katika
kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri
wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani
na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa
kuaminika;
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia
kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
husika.Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, - Cheti cha
mtihani wa Kidato cha IV na VI, - Computer Certificate, - Vyeti vya Kitaaluma
(Professional Certificate from Respective Boards);
vii. “Testmonial”, ‘‘Provisional Results”, “Statement of results”, hati ya matokeo ya Kidato
cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana
kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za
kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo
katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
x. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 24 Septemba, 2026.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na
vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: -
Ofisi ya Mkurugenzi, Mtaa wa Mtangani - Luganga, S.L.P. 76 Mafinga – Iringa: Simu: +255 026 2772393
Nukushi: +255 026 2772393 Barua pepe:td@mafingatc.go.tz; Tovuti: www.mafingatc.go.tz
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji Mafinga,
S.L.P. 76,
MAFINGA.
xi. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)
kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye
tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment
Portal'). Aidha, Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
Limetolewa na:
MKURUGENZI WA MJI
HALMASHAURI YA MJI
MAFINGA